_________________HABARI PAMOJA NA MAONI YA WASPMAJI WA MAGAZETI JUU YA ASKOFU_
Uadilifu Kiwe Kigezo Muhimu Zaidi Kuwa Kiongozi Tanzania Kwa Sasa!
Vatican yamvua jimbo Askofu
Imeandikwa na Mwandishi Wetu; Tarehe: 6th June 2009 @ 00:00 Imesomwa na watu: 3626; Jumla ya maoni: 32
Habari Zaidi:
• Basi laua watano Dodoma
• Mkutano wa Bunge waanza Dodoma
• Mahalu akwama, arudishwa Kisutu kujitetea
• Zitto kuishitaki HabariLeo
• Shahidi EPA augua ghafla kortini
• JK akutana na mabalozi wa Cuba, Saudia
• UDSM yafunga barabara hosteli Mabibo
• JK kuwahutubia wabunge kesho
• Watu 86 mbaroni uvamizi shambani kwa Kimaro
• Padri akemea ngono UDSM
• Wanne kizimbani kwa kuua albino
• Rasilimali fedha yatesa, yavigawa vyama
• Nyumba 12 zaongezwa fidia Mbagala
• Mhina atwaa kiti Wazazi CCM
• Kanisa Katoliki Same laelekea pabaya
• Mbunge Kimaro majaribuni tena
• Mauaji yafanyika hosteli za Mabibo
• Wafanyakazi TTCL ‘waisusia’ menejementi
• Kikwete aionya Jumuiya ya Wazazi
• Mabomu yadhibitiwa, 17 hoi kwa mshtuko
Habari zinazosomwa zaidi:
• Balaa lingine kwa Chenge
• Waliochaguliwa kujiunga kidato cha tano waongezeka kwa 22%
• Dina Marius, mrithi wa Amina Chifupa
• Salama: Jasiri aliyetangaza kuishi na virusi vya Ukimwi
• ‘Housigeli’ anataka kuniharibia ndoa
• Vatican yamvua jimbo Askofu
• Kikwete achekecha wakuu wa wilaya
• Orijino Komedi, Jay Dee waitwa Iringa
• Interpol yatumika kusaka wenye zeutamu
• JK apigilia msumari wa mwisho Dowans
Makao Makuu ya Kanisa Katoliki Vatican nchini Italia yamemnyang’anya Jimbo, Askofu wa Same, Jacob Koda, baada ya kubainika kukiuka mafundisho ya imani ya kanisa hilo. Balozi wa Vatican nchini, Askofu Mkuu Joseph Chennoth alithibitisha Dar es Salaam jana kuwa Askofu Koda ametakiwa na kanisa kuacha utume huo mara moja na kupumzika ama kufanya shughuli binafsi za mafunzo.
Hata hivyo, Balozi huyo wa Papa hakufafanua zaidi kiini cha kuondolewa kwa Askofu Koda na ni mafundisho gani ya kanisa aliyokiuka, ingawa taarifa kutoka Same zilizolifikia gazeti hili jana zilidai kuwa amejiingiza katika mafundisho yaliyo kinyume cha imani ya Kikristo na ya Kanisa Katoliki.
Sambamba na kuondolewa Askofu Koda katika jimbo hilo lililoko mkoani Kilimanjaro, pia taarifa ya Askofu Mkuu Chennoth kwa vyombo vya habari jana ilieleza kuwa Baba Mtakatifu Benedicto wa XVI amemteua Padri Rogath Kimaryo kuwa Msimamizi wa Kitume wa jimbo hilo hadi hapo litakapopata askofu mwingine.
Padri Kimaryo kabla ya uteuzi huo alikuwa Paroko wa Parokia ya Kipawa, Jimbo Kuu la Dar es Salaam. “Tumemshauri kuondoka jimboni na Padri Kimaryo ataongoza jimbo hilo kwa muda mpaka hapo Baba Mtakatifu atakapomteua askofu mpya,” alisema Askofu Mkuu Chennoth.
Aidha, taarifa hiyo ya Ubalozi wa Vatican hapa nchini kwa vyombo vya habari iliyotolewa kwa gazeti hili na Katibu Mtendaji wa Habari wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padri Revocatus Makonge, ilithibitisha uteuzi wa Padri Kimaryo katika jimbo hilo la Same.
“Mwakilishi wa Baba Mtakatifu hapa nchini anayo heshima kutangaza kuwa Baba Mtakatifu Benedicto wa XVI amemteua Padri Rogath Kimaryo (CSSP) ambaye ni Paroko wa Kipawa, Dar es Salaam kuwa Msimamizi wa Kitume mwenye mamlaka kamili na chini ya utii kwa kiti kitakatifu wa Jimbo Katoliki la Same,” ilieleza taarifa hiyo iliyotolewa Mei 30, mwaka huu. Hata hivyo, Padri Makonge alisema TEC haina taarifa zozote za kina kuhusu suala hilo na kueleza kuwa wanachofahamu ni uteuzi wa Padri Kimaryo kupitia taarifa hiyo ya Mwakilishi wa Papa nchini.
Taarifa zaidi kutoka katika ofisi za Ubalozi wa Vatican Dar es Salaam zilieleza kuwa Padri Kimaryo atakabidhiwa jimbo hilo kwa usimamizi rasmi kesho katika Ibada ya Misa itakayoongozwa na Mwadhama Polycarp Kadinali Pengo katika Kanisa Kuu la Same na kuhudhuriwa na viongozi kadhaa wa kanisa hilo akiwamo Askofu Mkuu Chennoth.
Bila kufafanua zaidi, Askofu Mkuu Chennoth alisema Kanisa Katoliki huwa lina utaratibu wa kumteua Msimamizi wa Jimbo linapotokea hitaji kama hilo hivyo ni kitu cha kawaida ndani ya kanisa pindi panapoonekana umuhimu wa kufanya hivyo.
Askofu Koda aliteuliwa na Baba Mtakatifu Yohane Paulo wa II kuwa Askofu Mpya wa Same Septemba 1999 kuchukua nafasi ya Askofu Josephat Lebulu aliyehamishiwa katika Jimbo Kuu la Arusha.
Padri Kimaryo ambaye ni Padri wa Shirika la Roho Mtakatifu alitunukiwa Udaktari wa Sheria nchini Roma katika Chuo Kikuu cha Pontifical Gregorian na pia amefanya kazi ya kitume kama mshauri kwa miaka sita katika nyumba yao ya shirika nchini humo.
Kwa utaratibu wa Kanisa Katoliki, Papa humteua Msimamizi wa Jimbo ambaye kikanisa ni kama Mtawala ambaye hufanya kazi hiyo, mara kadhaa hutumikia katika eneo ambalo halijapewa hadhi ya Jimbo au katika Jimbo lisilo na Askofu au tatizo kama lililotokea. Katika sheria za kanisa (Canon Law), utawala wa aina hiyo unampa mamlaka mtawala kufanya kazi zote za kiaskofu isipokuwa kuuza mali yoyote ya jimbo na kutoa daraja la upadrisho.
Jumal Maoni (32)
Maoni Tunaupongeza uongozi wa kanisa Katholiki lakini ni vizuri kuwa wazi huyo aliyefukuzwa kafanya nini? Labda kaonewa!
Maoni mimi naona taarifa hizi haziko sahihi kwa sababu hawajaweka wazi sheria iliyokiukwa, na hii ni kama kumnyima haki Askofu Koda au ni kuficha uovu wa kanisa au kwa namna nyingine kosa walilo mtuhumu linakosoa kanisa Katoliki na inaonekana hawajawa tayari kukosolewa mahubiri finyu wanayohubiri ambayo hayalingani na Biblia ilivyoandikwa
Maoni Hizi ni dalili tosha za mwisho wa dunia. Tuombe Mungu atusaidie.
Maoni Kwanza ninalishukuru kanisa kwa hatua iliyozichukua.
Lakini ninaomba pia kanisa liwe wazi kueleza sababu za msingi zilizo fanywa na mtumishi huyo wa Mungu ili iweze kuwa fundisho kwa wengine pia kulinda heshima na uadilifu wa kanisa kwa ujumla.
Maoni Naomba ufafanuzi zaidi juu ya hilo, kosa lake ni lipi na kanuni ya kanisa ni kusamehe? Ni bora kujua kosa kuliko kuficha maana wengine hawatajifunza.
Mungu anatuasa wanadamu kusamehe ina maana dhambi yake ni kubwa vipi hata asisamehewe?
Maoni Mi nadhani wangetueleza mafundisho gani ambayo amekiuka ya kikristo,isije ikawa na ubabe tu wa KIIMANI
Maoni Naomba Kanisa liwapitie Maaskofu wote . Mchunguzeni kwanza Askofu Josephat Lebulu wa Arusha. siku ya Pentekoste pale st. Theresa aliongoza ibada ambayo ilikiuka maadili ya ukatoliki kabisa ikawa kama ya kilokole (pentekoste) kila mtu anajifanya kashukiwa na roho mtakatifu zikaimbwa nyimbo ambazo si za kikatoliki. Tunaacha ukatoliki tunaenda kwenye madhehbu mengine
Maoni Tumuombe Mungu alisimamie kanisa lake. Shetani analitikisa lakini litasimama imara.
Maaskofu tujifunze kwa mifano hii. Atakayechezea nafasi yake atanyang'anywa.
Ikiwa maaskofu wanakuwa wazushi na wazinzi, je kanisa linakwenda wapi?
Asante Baba Mtakatifu kwa kuondoa mapadre na maaskofu wasiofaa.
Je walutheri, Waangalikana na madhehebu mengine ya Kikristo mnajifunza nini kwa hili la Askofu Jakob Koda. Tunajua wapo viongozi wa kanisa wamejiingiza kwenye uzinzi, wizi, biashara na hata ushirikina.
Kila mtu ataubeba mzigo wake mwenyewe.
Waumini
Jimbo la SAME
Maoni Kwa Jina la Allah mwingi wa rehema mwenye kuneemesha neema kubwa na mwenye kuneemesha neema ndogo.
Kwa jacob Koda,
Ushauri wangu kwako wewe ni kukubali Uislam. Kubali Uislam na utapata amani (ya dunia na akhera) na Allah atakupa malipo ya aina mbili.Ukikataa basi utajibebea madhambi yako na ya wale wanaokufuata.
Quran 3:64 64. Sema: Enyi Watu wa Kitabu (Wakristo na Mayahudi)! Njooni kwenye neno lilio sawa baina yetu na nyinyi: Ya kwamba tusimuabudu yeyote ila Mwenyezi Mungu, wala tusimshirikishe na chochote; wala tusifanyane sisi kwa sisi kuwa Waola Walezi badala ya Mwenyezi Mungu. Na wakigeuka basi semeni: Shuhudieni ya kwamba sisi ni Waislamu".
Maoni maskofu wa ainahiyo wako wengi hakuna mafundisho yanayo tolewa siku hizi ni kufatilia makanisa mengine na kwamba hata huku kwetu wapo tena hata mashehe wamemiliki misikiti kama mali yao . hata mimi naunga mkono vatcan inakuaje kwamba mchungaji au padri wanaendesha ibada huku waumini wamevalia mavazi mafupi kiasi kwamba hata anapoinama kusujudu mgongo unabaki wazi na kusababisha hata kwa wale wanaokua wamejifunga shanga zionekane kwa watu wasiohusika hata mbele za mungu ni uchafu. chukulia madhehebu ya kiroho yanay0fanya maombezi hufikia wakati waumini kuanguka chini huku kukiwa na umati mkubwa. maoni yangu viongozi wanaotangaza neno la mungu wawe makini wasije wakaongoza kondoo wa mungu ambao mungu atakuja kuahukumu kwenda jehanam NI MIMI MUAMINIFU KATIKA BWANA .MOURICE .TARIME
Maoni Kwanzakabisa nashukuru uongozi wa kanisa catholic kwa kua macho kuendelea kuchunguza mienendo ya watumishi wake,maranyingi tumekua tukisikia vituko wafanyavyo hao mapadri na maasikofu mpaka unajiuliza hao watu waliingia kwenye fani hiyo kwa kulazimishwa au vipi,kama atakua ameonekana na makosa basi wamuondoe ajichanganye mitaani.Maana wanakera sana kusimama madhabauni na kuongea maneno ya busara lakini wakitoka nje wanamega wake za watu,visichana vidogodogo nawengine kuwatia mimba wanafunzi.Ninawasiwasi nahuyo ASKOFU anaweza kua nae kakoboa vilevile nae akabolewe kwa njia nyingine Ahasanteni.
Maoni MAONI TUNGETOA KWA USAHIHI ZAIDI KAMA KOSA LAKE LINGEWEKWA WAZI,ILA KANISA HILI LINAWEZA LIKAKOSA MSIMAMO KWA VILE PIA LENYEWE HALISIMAMI KTK NENO, MFANO KUWEKA BAYANA KWAMBA POMBE SIO DHAMBI,JAMANI MAANDIKO YANAHITAJI UFAFANUZI WA KINA KWAKUWA NENO LASEMA 'ANDIKO HUUA LAKINI ROHO HUHUISHA'NA KAMA POMBE SIYO DHAMBI BEBA CHUPA YA BIA KATOE SADAKA,KWA UGUMU UTAKAOUSIKIA NDIO MAANA YA NENO HILI KWAMBA 'ANDIKO HUUA BALI ROHO HUHUISHA'MAANA YAKE KWAMBA YAPO MAANDIKO AMBAYO YANAHITAJI UFAFANUZI KTK ROHO SIYO TU KULIBEBA ANDIKO KAMA LILIVYO,HATA MTUME PETRO ALIKIRI KTK [2PETRO 3;16-17] WAZI KWAMBA KTK MAANDIKO YAPO MAMBO AMBAYO NI VIGUMU KUELEWA NAYO NA WATU WASIO NA ELIMU YA MUNGU HUYAPOTOSHA MUWE WAANGALIFU WAKATOLIKI FIKIRIE TENA KUHUSU KURUHUSU POMBE KITU AMBACHO KIKIMWINGIA KINAMBADISHA MAWZO NAKUFANYA CHOCHOTE.
Maoni In nominos patres et fillis et Sanctus spiritum, amesema baba mtakatifu kuna kitu ndani yake na iwe hivyo kwani Canon Laws zipo wazi na zinatoa mamlaka hayo kwake...
Ni matumaini ya wakristu wengi kuwa Askofu ajaye atakuwa mwema na mwenye kuheshimu ukristu na sheria takatifu za kanisa. Tuamini hivyo na iwe hivyo...
Maoni huu ni uonevu tu mbona kafanya mambo mengi mazuri jimboni. acheni wivu wa madaraka. msilete siasa katika kanisa la mungu
Maoni Sawa unamvua mtumishi/mtu madaraka na kueleza uma pasipo kueleza kwa kina chanzo cha kuvuliwa madaraka ama tuseme wito ambao hukaa ndani ya moyo. Ni bora walioweka mambo haya hadharani wangeweka na sababu ya tukio zima kwa ujumla wake ili waumini wasibaki na maswali yasiyo kuwa na majibu kutoka yanapostahili kwani tunaacha mwanya wa kuoneza majungu na kuchafuliana majina pasipo sababu.
Nawakilisha
William

Maoni Umefika wakati kanisa likawa lina tueleza ukweli wa makosa yalio tendwa ili nasi waumini tukiona mtumishi mwingine anatenda tujuwe hili nikosa. lakini kueleza makosa kwa ujumla 'kukiuka mafundisho ya imani ya kanisa' haitoshi. je makosa hayo ni yapi? baba wa taifa alisha sema mficha maradhi kilio kitamuumbua!
Tubadilike Kanisa Katoliki!!
Maoni kainisa katoliki linatakiwa kuwa makini sana kwani linamtazamo wa kiuchumi zaidi kuliko kiroho .kwani Waumini waleo niwadadisi wa mambo kuliko zamani ukiweka sheria watataka kujua ni kwanini tofauti nazamani walikua wanatii kwakutambua kua sheria ya kanisa nisheriaya mungu na hofu juu ya mungu imepungua kwa binadamu wa leo Kwahiyo kanisa lina hitaji kubadilika kutokana na mtazamo wakidunia
Kwa hiyo swala la kiroho linaonekana kama kigezo tu
Hata wachunga kondoo wa leo wanakwenda kinyume na maadili kutokana sera yenyewe kutokuwa wazi kwani kuna mambo mengiyamefichika wakitambua ukweli wake nndipo maadili yanapo vungika.Mfano. wahumini wa mwanzo hawakuruhusiwa kusoma biblia
hata ukisoma ni inglitu au agano jipya wazamani hawakuhoji ila wasasa niwadadisi sana .Tazama sasa waumini wengi hajui biblia na wanapo kabiliana na wanaojua wana potea kumbe nikuto kuelewa tu
Maoni Kanisa katoliki linamisingi mikuu mingi ikiwa ni pamoja na kutetea imani ya kikatoliki kama sala ya nasadiki inavyosisitiza
naafiki uamuzi wa baba mtakatifu kumteua mwingine ila nashauri ni vema tujue hasa askofu koda amekiuka kipi kwani mpaka sasa tupo kwenye mafumbo either baadhi ya wengine pengine watadhani kaonewa
Maoni Tunaomba tujulishwe huyu askofu Jacob Koda kakiuka mafundisho gani ya imani ya kanisa ? Jamani kuweni wawazi kwa waumini. mnatuficha nini ? Twambie tujue na tumwombee mtumishi wa bwana apate msamaa kwa Mungu , atubu na kupata wokovu.Kumbuka kuwa sisi sote tu wadhambi! yatupasa kutubu dhambi zetu na kuziacha kabisa ili tupate uzima wa milele.
Maoni Askofu koda pole kwa yaliyokusibu.kukosea na kutubu ndio mwanzo wa kusimama upya kiimani. koda kama ni uzinzi, au umetenda kosa kama alilofanya fr: kimaro, kuuza mali za kanisa.tubu
Maoni Askofu koda pole kwa yaliyokusibu.kukosea na kutubu ndio mwanzo wa kusimama upya kiimani. koda kama ni uzinzi, au umetenda kosa kama alilofanya fr: kimaro, kuuza mali za kanisa.tubu
Maoni taarifa hii ni ya kusikutisha na isitoshe inaamsha shauku ya kujua ni nini alichofanya kikubwa hadi kunyang'anywa Jimbo.
Maoni huwezi kumuhukumu mtu kwa kosa lisilo julikana lazima kujua kosa ndipo achukuliwe hatua ya kufukuzwa sikubaliani na kufukuzwa kwake mtu huyo lazima kujua kosa ndipo afukuzwe hatua kali zichukuliwe kuzalilishwa kwa askofu huyo nipotayari kua shahidi hata mbele za bwana kua hatujui kosa alilo lifanya zaidi ya wao kumuekea kashfa askofu huyo zaidi tunacho taka kujua kosa gani kwani hata yesu alisamehe watu bada yakujua kakosa kama muhalifu basi asemwe sinamengi ila maoni yatakamilika wakati tutajua kosa lake? napingavita sio vizuri kumtangazia mtu ubaya bila ya kujua kosalake hatari sana nduguzangu wa kikristo
yosia chimwai
kutoka zanzibar
Maoni Kanisa katoliki lina maongozi yake na walio ndani wanajua na km hawajui ni kosa lao. Yaliyotokea kwa askofu ni halali yake kwani alipoamua kazi ya kichungaji alitafakari kwanza.
Km kanisa halikumtendea haki anayo maamuzi mtendewa, na hii itategemea na maongozi ya kanisa.
Ni hiyari mtu kufuata akitakacho kwani dini si jambo jepesi km inavyodhaniwa na wengi kiasi imefikia mtu anasema mimi ni wa peponi na wewe ni wa motoni, ahsante kanisa katolki
Maoni unajua imani hizi za kuletewa zina matatizo yake na haya ni mwanzo tu.
Huyu askofu nisingependa kusena kuwa ana makosa au lah. sasa ametoa baraka kwa watu kibao je ndiyo kusema kuwa waliopewa baraka naye zimekuwa batili? Je mafundisho yake je?
Mimi ningependa kuwashauri watanzania wenzangu ni bora mkabaki kuwa Watanzania badala ya kuwa wafuasi wa Imani ambazo hakuna hata mmoja wetu mwenye mamlaka nazo.
Eti mimi ni muumini ambaye ninaamini Mungu lakini binadamu ndiyo wanaotoa hukumu kuwa hapa nimemkosea Mungu. Tufanye ibada tumuabudu Mungu achana na dini. zinapotosha kwani hawa wanaotuongoza ni 100% binadamu, wana mapungufu yao.
Hata huyo Papa, pia ana mapungufu.please, turudi katika imani za asili tuishi.
Maoni Wakristo wenzangu, kanisa la katoliki lina misingi na taratibu zake za kuongoza na kuwaweka wakfu na kuwaondolea wakfu watumishi wake. Hili lililompata Askofu lisitumike kama mwanya wa kukejeli imani ya kikatoliki au imani nyingine. Hawa viongozi wa imani mbalimbali tulizonazo hawakushuka kutoka juu, bali ni binadamu kama sisi, wenye miili dhaifu kama yetu na wanaitafuta mbingu kama wewe na mimi. Hawa ni kama madereva tu ambao gari likianguka na yeye anakufa au kujeruhiwa kama abiria yeyote. Hivyo kwa waumini bora huu ni wakati wa kuwaombea wacha Mungu wote wadumu kuwa imara katika imani hiyo na siyo kutumia udhaifu wa viongozi wa kidini kama kigezo cha kuchafua imani. Kama Askofu huyo kaonewa, yeye mwenyewe kwa mujibu wa taratibu za kanisa hilo atakata rufaa. Tuwaache viongozi wa kanisa hilo wafanye kazi yao.
Mshauri wa watoa maoni
Ireland
Maoni pole askofu koda kwa yaliokusibu, usijali yatapika.ulichokosa tubu na mungu atakusamehe,ila kanisa katolilik msiwe mafya kiasi hicho elezen ukwel alichokosa.Najua umefanya mema mengi na mabaya mengi koda il a si wewe tu ni wengi mapadr na maaskof wamefanya makosa, mbona wao wamesamehewa?nataman kuandika makala kutokana na tukio hili kwan limenigusa sana na ukizingatiwa mimi ni mkatoloki wa damu, ila maadil ya kikatolik yanakandamiza baadhi ya watu,kuen wakwel semen makosa yake.
kuwen wawaz,wote ni binadamu na tunakosa ila tusameheane.
Maoni Waweke wazi sababu ya kufuzwa kama walivyoweka wazi kumuachisha. Mimi sidhani kama ni sawa walichofanya kwani hawa viongozi wetu wa RC... MHH! Wananishangaza sana na matendo yao, Kama kweli Mungu yupo, basi nimeamini usemi usemao "Mungu si Athumani"
Kikubwa... "Asiyekuwa na dhambi basi awe wa kwanza kumtupia jiwe mwenzake..."
Inasikitisha kwakweli, ingawa sijui alichokifanya, ila hawa viongozi wa RC sio wote wenye matendo mema.
Maoni Watu wanashauku sana kujua makosa ya wenzao, halafu sijui ili iweje.
Mimi naona si vema wala busara kung'ang'ania kujua makosa ya wengine wakati sisi wenyewe tuna makosa yetu, tena mengine yanayotia hata kinyaa mbele za Mungu na wenzetu. Tunapenda sana kuwa mashabiki wa makosa ya wenzetu ili kuwanyoshea vidole.
Kanisa linafanya vema kwa kutotangaza makosa ya Askofu Koda ili kuondoa unyanyapaa wa watu wanaopenda kuwatupia wenzao mawe kana kwamba ni wakosefu wakubwa kuliko wao.
Yatosha mtu kujua dhambi zako mwenyewe na kuomba msamaha wa Mungu kwa ajili yako mwenyewe. Na Askofu Koda lazima anayajua makosa yake mwenyewe (au amejulishwa na Kanisa makosa yake) na tunamuombea Mungu amjalie neema ya kuyatubia.
Kwa Kanisa kufikia uamuzi mkubwa hivyo ni lazima limefanya uchunguzi wa kina (hata pengine kujadiliana na mhusika kwa kina) na limejiridhisha na hali ya mambo. Zaidi sana limeona madhara yake kwa Kanisa la Same siku za baadae. Tuliamini Kanisa.
Wakati tunapong'ang'ania kujua makosa ya wengine tukumbuke maneno ya Bwana Yesu "Anayejiona hana dhambi awe wa kwanza kumtupia huyu mwanamke jiwe" (Yohane 8:7).
Vilevile tuache tabia ya Kulitupia lawama Kanisa zima kwa makosa ya baadhi ya waamini wake; kama vile hatuwezi kuwatupia lawama mitume wote kwa kosa la Yuda Iskariote. Kanisa haliachi kuwa la kweli kwa vile miongoni wa waamini wake ni wadhambi! Wadhambi ktk Kanisa walikuwepo tangu karne ya kwanza (rejea Barua za Mitume katika Biblia hasa za Mtume Paulo na Pia Kitabu cha Ufunuo; nyaraka kwa makanisa saba). Na ndio maana kuna siku ya hukumu ambapo uzuri na ubaya wa kila mtu utafunuliwa. Na miongoni mwetu tunaofunua sana midomo yetu tutaumbuliwa siku ile. Basi tuache kushabikia makosa ya wenzetu, yetu yanatutosha. Tuache kulaumiana na kuhukumiana kama alivyotuasa Bwana Yesu mwenyewe.
Bwana atujalie Roho wa Hekima na Akili tujue nafasi zetu katika njia ya wokovu; na tumwachie Mungu yaliyo ya Mungu.
Maoni Mimi ni muumini katika jimbo katoliki la Same Parokia ya Yesu Mwenye Huruma - Mwanga, imeniuma sana. Binafsi naona taarifa hizi haziko sahihi na maoni mengi yanayotolewa huenda nayo yasiwe sahihi kwa sababu hawajaweka wazi maadili yaliyokiukwa, na hii ni kama kumnyima haki Askofu Koda au ni kuficha uovu wa kanisa au kwa namna nyingine kosa walilo mtuhumu linakosoa kanisa Katoliki na inaonekana hawajawa tayari kukosolewa.
Mimi naafiki uamuzi wa Baba Mtakatifu kumteua Msimamizi mwingine ila nashauri ni vema tujue hasa askofu Koda amekiuka kipi kwani mpaka sasa tupo kwenye mafumbo either baadhi ya wengine pengine watadhani kaonewa na makosa hayo hayo yanaweza kuendelea kujitokeza.
Maoni kanisa katoliki lina tatizo kubwa la usiri na hapa linapaswa kubadilika.makosa ya askofu koda hayakuwekwa wazi hata hivyo kuna tatizo la ukosefu wa maadili kwa baadhi ya watumishi wake
GAZETI LA HABARI LEO JUU YA ASKOFU KODA
Makao Makuu ya Kanisa Katoliki Vatican nchini Italia yamemnyang’anya Jimbo, Askofu wa Same, Jacob Koda, baada ya kubainika kukiuka mafundisho ya imani ya kanisa hilo. Balozi wa Vatican nchini, Askofu Mkuu Joseph Chennoth alithibitisha Dar es Salaam jana kuwa Askofu Koda ametakiwa na kanisa kuacha utume huo mara moja na kupumzika ama kufanya shughuli binafsi za mafunzo.
Hata hivyo, Balozi huyo wa Papa hakufafanua zaidi kiini cha kuondolewa kwa Askofu Koda na ni mafundisho gani ya kanisa aliyokiuka, ingawa taarifa kutoka Same zilizolifikia gazeti hili jana zilidai kuwa amejiingiza katika mafundisho yaliyo kinyume cha imani ya Kikristo na ya Kanisa Katoliki.
Sambamba na kuondolewa Askofu Koda katika jimbo hilo lililoko mkoani Kilimanjaro, pia taarifa ya Askofu Mkuu Chennoth kwa vyombo vya habari jana ilieleza kuwa Baba Mtakatifu Benedicto wa XVI amemteua Padri Rogath Kimaryo kuwa Msimamizi wa Kitume wa jimbo hilo hadi hapo litakapopata askofu mwingine.
Padri Kimaryo kabla ya uteuzi huo alikuwa Paroko wa Parokia ya Kipawa, Jimbo Kuu la Dar es Salaam. “Tumemshauri kuondoka jimboni na Padri Kimaryo ataongoza jimbo hilo kwa muda mpaka hapo Baba Mtakatifu atakapomteua askofu mpya,” alisema Askofu Mkuu Chennoth.
Aidha, taarifa hiyo ya Ubalozi wa Vatican hapa nchini kwa vyombo vya habari iliyotolewa kwa gazeti hili na Katibu Mtendaji wa Habari wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padri Revocatus Makonge, ilithibitisha uteuzi wa Padri Kimaryo katika jimbo hilo la Same.
“Mwakilishi wa Baba Mtakatifu hapa nchini anayo heshima kutangaza kuwa Baba Mtakatifu Benedicto wa XVI amemteua Padri Rogath Kimaryo (CSSP) ambaye ni Paroko wa Kipawa, Dar es Salaam kuwa Msimamizi wa Kitume mwenye mamlaka kamili na chini ya utii kwa kiti kitakatifu wa Jimbo Katoliki la Same,” ilieleza taarifa hiyo iliyotolewa Mei 30, mwaka huu. Hata hivyo, Padri Makonge alisema TEC haina taarifa zozote za kina kuhusu suala hilo na kueleza kuwa wanachofahamu ni uteuzi wa Padri Kimaryo kupitia taarifa hiyo ya Mwakilishi wa Papa nchini.
Taarifa zaidi kutoka katika ofisi za Ubalozi wa Vatican Dar es Salaam zilieleza kuwa Padri Kimaryo atakabidhiwa jimbo hilo kwa usimamizi rasmi kesho katika Ibada ya Misa itakayoongozwa na Mwadhama Polycarp Kadinali Pengo katika Kanisa Kuu la Same na kuhudhuriwa na viongozi kadhaa wa kanisa hilo akiwamo Askofu Mkuu Chennoth.
Bila kufafanua zaidi, Askofu Mkuu Chennoth alisema Kanisa Katoliki huwa lina utaratibu wa kumteua Msimamizi wa Jimbo linapotokea hitaji kama hilo hivyo ni kitu cha kawaida ndani ya kanisa pindi panapoonekana umuhimu wa kufanya hivyo.
Askofu Koda aliteuliwa na Baba Mtakatifu Yohane Paulo wa II kuwa Askofu Mpya wa Same Septemba 1999 kuchukua nafasi ya Askofu Josephat Lebulu aliyehamishiwa katika Jimbo Kuu la Arusha.
Padri Kimaryo ambaye ni Padri wa Shirika la Roho Mtakatifu alitunukiwa Udaktari wa Sheria nchini Roma katika Chuo Kikuu cha Pontifical Gregorian na pia amefanya kazi ya kitume kama mshauri kwa miaka sita katika nyumba yao ya shirika nchini humo.
Kwa utaratibu wa Kanisa Katoliki, Papa humteua Msimamizi wa Jimbo ambaye kikanisa ni kama Mtawala ambaye hufanya kazi hiyo, mara kadhaa hutumikia katika eneo ambalo halijapewa hadhi ya Jimbo au katika Jimbo lisilo na Askofu au tatizo kama lililotokea. Katika sheria za kanisa (Canon Law), utawala wa aina hiyo unampa mamlaka mtawala kufanya kazi zote za kiaskofu isipokuwa kuuza mali yoyote ya jimbo na kutoa daraja la upadrisho.
Source: Habari Leo
GAZETI LA MWANANCHI
LINAELEZA KAMA IFUATAVYO
Re: Vatican yamvua jimbo Askofu
________________________________________
Askofu aliyevuliwa madaraka Same akana kushiriki Freemason
Jimbo Katoliki la Same, amejitokeza hadharani na kuweka wazi na kiini cha hatua hiyo huku akikanusha taarifa zilizozagaa kuwa anashiriki dini ya mashetani.
Akizungumza katika mahojiano maalumu na Mwanachi Jumapili jana alisema, “Sijashiriki na sitashiriki dini hiyo, lakini wanaozusha hayo mambo wajue muosha naye huoshwa, hivyo walivyonisingizia siku sio nyingi vitawarudi”.
Kulingana na taarifa hizo, kuvuliwa madaraka kwa Askofu Koda kumetokana na madai ya kujihusisha na dini ya kishetani (Freemason) na kwamba mwenendo huo ulibainika katika uchunguzi wa kishushushu uliofanywa na kanisa kwenye makazi ya askofu huyo.
Lakini taarifa iliyotolewa na Ubalozi wa Vatican jijini Dar es salaam juzi na kukaririwa na vyombo vya habari haikufafanua kisa cha kuondolewa kwake mamlaka zaidi ya kusema tu kuwa amebainika kukiuka mafundisho ya kanisa hilo.
Baba Mtakatifu Benedicto wa XVI amemteua Padri Rogath Kimaryo, Paroko wa Parokia ya Kipawa, Jimbo Kuu la Dar es Salaam kuwa Msimamizi wa Kitume wa jimbo hilo hadi hapo litakapopata askofu mwingine.
Padri Kimaryo anakabidhiwa jimbo hilo kwa usimamizi rasmi leo katika Ibada ya Misa itakayoongozwa na Mwadhama Polycarp Kadinali Pengo katika Kanisa Kuu la Same na kuhudhuriwa na viongozi kadhaa wa kanisa hilo akiwamo Balozi wa Vatican, Askofu Mkuu Joseph Chennoth.
Askofu Koda ambaye hata hivyo alisisitiza kuwa yeye bado ni askofu hadi milele kwa kuwa alichoondolewa ni mamlaka ya kuongoza jimbo, alifafanua kuwa hatua hiyo dhidi yake inatokana na uchu wa madaraka, chuki binafsi na wivu wa maendeleo aliyoleta katika jimbo hilo.
Alisema wenye uchu wa madaraka na ambao wamejilimbikizia mali wameungana na askofu mmoja mwandamizi kwenye Kanda ya Kaskazini kumchafua.
Kwa mujibu wa Koda, Askofu huyo anadaiwa kujenga chuki binafsi na wivu na aliouonyesha waziwazi wakati yeye (Koda) alipomwalika Rais Kikwete kufungua shule ya wasichana ya Kandoto.
Kabla ya kuzungumza na gazeti hili ilimlazimu kwanza kutoa dukuduku lake kuwa yeye hajalikimbia jimbo hilo.
“Kwanza napenda kusema kwamba si kweli kwamba sijulikani nilipo kama gazeti lilivyosema (sio Mwananchi) kama ningekuwa sijulikani nilipo kanisa lingepeleka taarifa polisi nao wangeanza kunitafuta,” alisema Askofu Koda.
Askofu Koda alisema kwa wiki nzima amekuwa jimboni humo akiendesha ibada na kwamba, jana asubuhi aliendesha ibada katika kanisa la Mtakatifu Bernard na kwamba hawezi kulikimbia jimbo hilo kamwe.
Akifafanua zaidi kile anachodai ni wivu dhidi yake, alisema “Kiongozi wa kanisa (anamtaja) alionyesha kutofurahishwa na mimi kumwalika Rais Kikwete na hata kabla ya siku yenyewe aliniuliza kwanini nimemwalika rais ambaye ni Muislamu kufungua shule ya kanisa,” alisema Askofu Koda.
Askofu huyo anasema alikataa ushauri wa kiongozi huyo na tangu wakati huo alianza kumzulia mambo mengi akihoji zilikopatikana fedha zilizotekeleza miradi mikubwa jimboni humo.
Baadhi ya miradi ambayo Koda anadai inaonewa wivu na kiongozi huyo, ni Seminari ya Chanjale, shule za Dido, Vumari, Kandoto, Mother Theresa of Calcutta na nia yake ya kutaka kujenga chuo kikuu jimboni kwake.
Kwa mujibu wa Askofu Koda, mafanikio makubwa yaliyopatikana katika uongozi wake ni pamoja na kusomesha mapadri 34 nje ya nchi, 19 kwa ngazi ya Shahada za Uzamivu (PhD) ni baadhi ya mambo yaliyoibua mambo yote hayo.
Hata hivyo, pamoja na vikwazo hivyo bado anayo mipango kabambe ya baadaye ili kulifanya jimbo hilo lifikie katika hali ya kujitegemea katika suala la rasilimali watu na kutoa mchango kwa Same na taifa kwa ujumla.
Alieleza kuwa mpango wake wa kuanzisha chuo Kikuu cha Ngalekeru katika Wilaya za Same na Mwanga uko katika hatua nzuri na Chuo Kikuu cha California nchini Marekani kimekubali kuanza ujenzi huo Septemba mwaka huu.
Askofu Koda alisema kuwa mpango mwingine wa kuanzisha hospitali kubwa ambayo ingekuwa na chuo cha madaktari wilayani Mwanga ambayo ingekuwa chini ya Hospitali ya Saint Raphael ya Milano nchini Italia.
“Mipango yote hii imeibua maswali yenye wivu kwamba hizo pesa zinatoka wapi,” alisema Askofu Koda bila kusema kama fedha hizo ndizo zinazodaiwa kutoka katika dini ya mashetani kama uvumi ulivyoenezwa.
Askofu huyo alisisitiza kuwa lengo lake ni kunyanyua jamii ya Upare hasa ikizingatiwa kuwa Upare ni pakavu, hivyo mchango wa shule na miradi mingine mikubwa ingesaidia kuleta mabadiliko ya kiuchumi.
Mwandishi wa Habari wa Idara ya mawasiliano ya Jimbo, Padri Joseph Mlacha alisema taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari imepotosha umma.
“Alichoondolewa Askofu ni Mamlaka ya Jimbo tu lazima ifahamike kuwa Uaskofu Sakramenti daraja la tatu, huwa unadumu milele na ndio maana Askofu amewasiliana na wanasheria wake,” alisema.
Source: Mwananchi
MAONI YA WANANCHI MBALI MBALI
Akifafanua zaidi kile anachodai ni wivu dhidi yake, alisema “Kiongozi wa kanisa (anamtaja) alionyesha kutofurahishwa na mimi kumwalika Rais Kikwete na hata kabla ya siku yenyewe aliniuliza kwanini nimemwalika rais ambaye ni Muislamu kufungua shule ya kanisa,” alisema Askofu Koda.
No! No! Kanisa haliwezi kumkataa kiongozi wa nchi kwani imeandikwa watii viongozi, ila labda kwa sababu Kikwete analea mafisadi na hivyo kuwa mfano mbaya kwa waumini wa dini anaweza kukataliwa asihudhurie mikusanyiko ya kanisa kwani itakuwa picha mbaya kuenzi wahalifu na haya sio mafundisho ya kanisa, inampasa Kikwetekukusanyika kwenye makundiya akina Rostam, lowasa, chenge nk.
Askofu huyo anasema alikataa ushauri wa kiongozi huyo na tangu wakati huo alianza kumzulia mambo mengi akihoji zilikopatikana fedha zilizotekeleza miradi mikubwa jimboni humo.
Kama chanzo cha fedha hakijulikani ni lazima kanisa lihoji
Baadhi ya miradi ambayo Koda anadai inaonewa wivu na kiongozi huyo, ni Seminari ya Chanjale, shule za Dido, Vumari, Kandoto, Mother Theresa of Calcutta na nia yake ya kutaka kujenga chuo kikuu jimboni kwake.
Uongo uongo,
Chanjale seminari na Dido vilikuwepo zamani sana miaka ya 1984 wakati huo koda alikuwa seminari anasoma level ya chini kabisa.wakati huo askofu Josephati Lebulu ndiye alikuwa askofu na mwanzilishi wa hizi seminari jimboni same.Sina kumbu kumbu na hizo nyingine
Kwa mujibu wa Askofu Koda, mafanikio makubwa yaliyopatikana katika uongozi wake ni pamoja na kusomesha mapadri 34 nje ya nchi, 19 kwa ngazi ya Shahada za Uzamivu (PhD) ni baadhi ya mambo yaliyoibua mambo yote hayo.
Si kweli kwani ni kawaida ya majimbo kusomesha mapdri hata yeye Koda alisomeshwa na wengine wengi. hata hivyo haiongezi kitu sana ikizingatiwa kazi kubwa ni kumtumikia mungu na waumini kwa unyenyekevu sio cheo au dhamana. Mapadri wengi tanzania wana phd.
Hata hivyo, pamoja na vikwazo hivyo bado anayo mipango kabambe ya baadaye ili kulifanya jimbo hilo lifikie katika hali ya kujitegemea katika suala la rasilimali watu na kutoa mchango kwa Same na taifa kwa ujumla.
waumini hutoa sadaka na zaka, jimbo kuwa tajiri inatokana na vipato vya waumini na jinsi watakavyoitikia kutoa saka na zaka, ni kazi ya jimbo kupigia kelele uongozi wa kimaendeleo wa serikali ili kuwezesha wananchi wote kuwa na maisha dhabiti ya kujitegemea na kutokana na umasikini.
Alieleza kuwa mpango wake wa kuanzisha chuo Kikuu cha Ngalekeru katika Wilaya za Same na Mwanga uko katika hatua nzuri na Chuo Kikuu cha California nchini Marekani kimekubali kuanza ujenzi huo Septemba mwaka huu.
Askofu Koda alisema kuwa mpango mwingine wa kuanzisha hospitali kubwa ambayo ingekuwa na chuo cha madaktari wilayani Mwanga ambayo ingekuwa chini ya Hospitali ya Saint Raphael ya Milano nchini Italia.
“Mipango yote hii imeibua maswali yenye wivu kwamba hizo pesa zinatoka wapi,” alisema Askofu Koda bila kusema kama fedha hizo ndizo zinazodaiwa kutoka katika dini ya mashetani kama uvumi ulivyoenezwa.
Basi aseme vyanzo vya fedha, kwani Jimbo la same ni jimbo la wakatoliki wa jimbo la same miradi yote ya kanisa duniani kote vyanzo vya fedha vipo wazi na chanzo kikubwa ni michango ya waumini na kila muumini anajua kwamba sasa tunachangia hiki au kile na kama kuna misaada inatangazwa wazi na mapato yote ya jimbo yanayotokana na miradi ya jimbo huwekwa wazi. sasa Baba askofu Koda ana maswali ya kujibu hizo fedha anatoa wapi, hatari zaidi amehusishwa kwenye biashara ya drugs, na dini ya mashetani, sijui ushiriki wake unakuwaje hapa ila anatakiwa kutoa majibu sio kujitetea
Askofu huyo alisisitiza kuwa lengo lake ni kunyanyua jamii ya Upare hasa ikizingatiwa kuwa Upare ni pakavu, hivyo mchango wa shule na miradi mingine mikubwa ingesaidia kuleta mabadiliko ya kiuchumi.
Mwandishi wa Habari wa Idara ya mawasiliano ya Jimbo, Padri Joseph Mlacha alisema taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari imepotosha umma.
“Alichoondolewa Askofu ni Mamlaka ya Jimbo tu lazima ifahamike kuwa Uaskofu Sakramenti daraja la tatu, huwa unadumu milele na ndio maana Askofu amewasiliana na wanasheria wake,” alisema.
Inakuwaje leo baba askofu Koda kwenda kwa mwanasheria ili aendelee kuwa askofu, haya sio mafundisho ya dini wala ya daraja la upadri na uaskofu, madaraja haya yanafundisha utii, kama wamekuona haufai ni haufai. Ni mafundisho ya kanisa kuwa likifungiwa duniani na mbinguni ni hivyo hivyo hakuna rufaa kwenye dini ndio maana hata maungamo hayana rufaa inaaminika ni kufunguliwa mbinguni. Sasa baba askofu umeonekana hufai kulea kondoo wa bwana ila nawe unatakiwa kulelewa, hata yesu alichukua baadhi kufuga kondoo wake hakuchukuwa wote, hata hivyo kati ya wale kumi na wawili mmoja alitemwa Yuda ambaye tamaa ilimtawala, usiogope tukae wite kwenye bench nasi tupokee somo ili tufike mbinguni juu kwa baba huko hakuna askofu wala padri hakuna tajiri wala masikini kila kitu ni mswano.
Pamoja na haya yote ulileta mshangao mkubwa sana pale ulipotangazwa kuwa wewe ni askofu mwaka 1999, nilistaajabu na sikuchelea kuamini kuwa hizi ni mbio za sakafuni. Kumbuka ulivyokuwa seminari, na kumbuka ulivyokuwa padri je uliwacha yale yote, inawezekana uliendeleza, nakushauri usiendelee kupiga kelele kwani yakiwekwa hadharani itakuwa mbaya sana. Nakutakia maisha mema ya kitume kwa ngazi yeyote ile.
__________________
Tanzania itakuwa huru wananchi wakimiliki nchi yao wenyewe sio baadhi ya wateule wachache.Haki na sheria kwa wote bila kujali rangi,cheo,na utajiri wa mtu.
The Following User Says Thank You to kinepi_nepi For This Useful Post:
Masanilo (7th June 2009)
#17 (permalink)
7th June 2009, 06:16 AM
Abdulhalim
Abdulhalim is the same voice of reason.
JF Senior Expert Member Join Date: Fri Jul 2007
Posts: 3,701
Thanks: 82
Thanked 110 Times in 81 Posts
Rep Power: 29
Credits: 327,855
Re: Vatican yamvua jimbo Askofu
________________________________________
Quote: kinepi_nepi
Pamoja na haya yote ulileta mshangao mkubwa sana pale ulipotangazwa kuwa wewe ni askofu mwaka 1999, nilistaajabu na sikuchelea kuamini kuwa hizi ni mbio za sakafuni. Kumbuka ulivyokuwa seminari, na kumbuka ulivyokuwa padri je uliwacha yale yote, inawezekana uliendeleza, nakushauri usiendelee kupiga kelele kwani yakiwekwa hadharani itakuwa mbaya sana. Nakutakia maisha mema ya kitume kwa ngazi yeyote ile.
ololololol...mazee inaonekana nyie ni waarabu wa Pemba.. sasa kwa nini mkuu na wewe usimwage ugali, maana baba askofu kesha mwaga mboga. Si unajua hapa ni JF where we dare to talk sense OPENLY..?
__________________
Why they don't get a ni99a like me to sing the national anthem?
#18 (permalink)
7th June 2009, 08:25 PM
Ndahani
Ndahani has no status.
Senior Member Join Date: Tue Jun 2008
Posts: 219
Thanks: 14
Thanked 72 Times in 52 Posts
Rep Power: 22
Credits: 705,165
Re: Vatican yamvua jimbo Askofu
________________________________________
Quote: Next Level
TEC lazima watakuwa wanajua in and out ya issue hii, haiwezekani huo ukikwaji ukawa noted Vatican wakati hapa kuna Cardinal Pengo ambaye ndio mkuu wa RC hapa Tz....so kama askofu Koda anatatizo, basi itakuwa ni mkuu wake kamrepoti kwa papa na si vinginevyo!
Kama ile habari ya mwananchi la leo iko sahihi, sidhani ni Cardinal ndo aliyemripoti.Itakuwa ni huko huko same maana wanahisi ni freemason member. Ninachohisi, kuna makubwa zaidi yapo yafichwafichwa. Time will tell
#19 (permalink)
7th June 2009, 08:30 PM
Ndahani
Ndahani has no status.
Senior Member Join Date: Tue Jun 2008
Posts: 219
Thanks: 14
Thanked 72 Times in 52 Posts
Rep Power: 22
Credits: 705,165
Re: Vatican yamvua jimbo Askofu
________________________________________
Quote: kinepi_nepi
Pamoja na haya yote ulileta mshangao mkubwa sana pale ulipotangazwa kuwa wewe ni askofu mwaka 1999, nilistaajabu na sikuchelea kuamini kuwa hizi ni mbio za sakafuni. Kumbuka ulivyokuwa seminari, na kumbuka ulivyokuwa padri je uliwacha yale yote, inawezekana uliendeleza, nakushauri usiendelee kupiga kelele kwani yakiwekwa hadharani itakuwa mbaya sana. Nakutakia maisha mema ya kitume kwa ngazi yeyote ile.
Yapi hayo mkuu tuhabarishe...Kuna habari kuwa baadhi ya viongozi wa juu wa kanisa katoliki TZ, kuna freemasons.Is it one of them
Saturday, 6 June 2009

----------------------------------------------------------------------------
HABARI KUTOKA VATICAN
Makao Makuu ya Kanisa Katoliki Vatican nchini Italia yamemnyang’anya Jimbo, Askofu wa Same, Jacob Koda, baada ya kubainika kukiuka mafundisho ya imani ya kanisa hilo. Balozi wa Vatican nchini, Askofu Mkuu Joseph Chennoth alithibitisha Dar es Salaam jana kuwa Askofu Koda ametakiwa na kanisa kuacha utume huo mara moja na kupumzika ama kufanya shughuli binafsi za mafunzo.
Hata hivyo, Balozi huyo wa Papa hakufafanua zaidi kiini cha kuondolewa kwa Askofu Koda na ni mafundisho gani ya kanisa aliyokiuka, ingawa taarifa kutoka Same zilizolifikia gazeti hili jana zilidai kuwa amejiingiza katika mafundisho yaliyo kinyume cha imani ya Kikristo na ya Kanisa Katoliki.
Sambamba na kuondolewa Askofu Koda katika jimbo hilo lililoko mkoani Kilimanjaro, pia taarifa ya Askofu Mkuu Chennoth kwa vyombo vya habari jana ilieleza kuwa Baba Mtakatifu Benedicto wa XVI amemteua Padri Rogath Kimaryo kuwa Msimamizi wa Kitume wa jimbo hilo hadi hapo litakapopata askofu mwingine.
Padri Kimaryo kabla ya uteuzi huo alikuwa Paroko wa Parokia ya Kipawa, Jimbo Kuu la Dar es Salaam. “Tumemshauri kuondoka jimboni na Padri Kimaryo ataongoza jimbo hilo kwa muda mpaka hapo Baba Mtakatifu atakapomteua askofu mpya,” alisema Askofu Mkuu Chennoth.
Aidha, taarifa hiyo ya Ubalozi wa Vatican hapa nchini kwa vyombo vya habari iliyotolewa kwa gazeti hili na Katibu Mtendaji wa Habari wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padri Revocatus Makonge, ilithibitisha uteuzi wa Padri Kimaryo katika jimbo hilo la Same.
“Mwakilishi wa Baba Mtakatifu hapa nchini anayo heshima kutangaza kuwa Baba Mtakatifu Benedicto wa XVI amemteua Padri Rogath Kimaryo (CSSP) ambaye ni Paroko wa Kipawa, Dar es Salaam kuwa Msimamizi wa Kitume mwenye mamlaka kamili na chini ya utii kwa kiti kitakatifu wa Jimbo Katoliki la Same,” ilieleza taarifa hiyo iliyotolewa Mei 30, mwaka huu. Hata hivyo, Padri Makonge alisema TEC haina taarifa zozote za kina kuhusu suala hilo na kueleza kuwa wanachofahamu ni uteuzi wa Padri Kimaryo kupitia taarifa hiyo ya Mwakilishi wa Papa nchini.
Taarifa zaidi kutoka katika ofisi za Ubalozi wa Vatican Dar es Salaam zilieleza kuwa Padri Kimaryo atakabidhiwa jimbo hilo kwa usimamizi rasmi kesho katika Ibada ya Misa itakayoongozwa na Mwadhama Polycarp Kadinali Pengo katika Kanisa Kuu la Same na kuhudhuriwa na viongozi kadhaa wa kanisa hilo akiwamo Askofu Mkuu Chennoth.
Bila kufafanua zaidi, Askofu Mkuu Chennoth alisema Kanisa Katoliki huwa lina utaratibu wa kumteua Msimamizi wa Jimbo linapotokea hitaji kama hilo hivyo ni kitu cha kawaida ndani ya kanisa pindi panapoonekana umuhimu wa kufanya hivyo.
Askofu Koda aliteuliwa na Baba Mtakatifu Yohane Paulo wa II kuwa Askofu Mpya wa Same Septemba 1999 kuchukua nafasi ya Askofu Josephat Lebulu aliyehamishiwa katika Jimbo Kuu la Arusha.
Padri Kimaryo ambaye ni Padri wa Shirika la Roho Mtakatifu alitunukiwa Udaktari wa Sheria nchini Roma katika Chuo Kikuu cha Pontifical Gregorian na pia amefanya kazi ya kitume kama mshauri kwa miaka sita katika nyumba yao ya shirika nchini humo.
Kwa utaratibu wa Kanisa Katoliki, Papa humteua Msimamizi wa Jimbo ambaye kikanisa ni kama Mtawala ambaye hufanya kazi hiyo, mara kadhaa hutumikia katika eneo ambalo halijapewa hadhi ya Jimbo au katika Jimbo lisilo na Askofu au tatizo kama lililotokea. Katika sheria za kanisa (Canon Law), utawala wa aina hiyo unampa mamlaka mtawala kufanya kazi zote za kiaskofu isipokuwa kuuza mali yoyote ya jimbo na kutoa daraja la upadrisho.
Source: Habari Leo
Kwa wanaojua Askofu Koda ni mafundisho gani ya kanisa aliyokiuka ? TAFADHARI WATUME KWA WEBSITE AUTHOR
Subscribe to:
Posts (Atom)